KATIBA YA KIKUNDI CHA PAMOJA TUNAWEZA.
UTANGULIZI:
(PAMOJA TUNAWEZA) - Ni kikundi cha hiari chenye
lengo la kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa ustawi wa
wanachama wake. Kikundi hiki kimeanzishwa rasmi tarehe..........
Kwa pamoja wanachama wanaahidi kuilinda na kuitekeleza katiba hii.
Pamoja na Katiba hii, Kikundi hiki kitaendeshwa kwa
mujibu wa kanuni mbalimbali ambazo zitawekwa na wanachama.
SURA YA KWANZA
1.
JINA LA KIKUNDI, ANUANI
YA KIKUNDI NA TAFSIRI
1.1. JINA LA KIKUNDI
Kikundi hiki kitajulikana kama PAMOJA TUNAWEZA.
Anuani ya kikundi hiki itakuwa ni sanduku la barua S.L.P 90315 DAR ES SALAAM.
Anuani ya makazi ambayo ni Makao Makuu ya Kikundi hiki
yatakuwa ni …KATA-MZIMUNI. Mtaa wa MTAMBANI......
Wilaya-KINONDONI
1.2 TAFSIRI
Kwa mujibu wa Katiba hii, maneno yafuatayo yatakuwa na
maana ifuatayo;
(i)
Mwanachama: Mtu yeyote atakayekidhi vigezo vya kuwa mwanachama
(ii)
Mwanachama hai : Mwanachama anayetimiza masharti ya kuwa mwanachama kwa
mujibu wa katiba hii.
(iii)
Kanuni: Muongozo
wa jinsi ya uendendeshaji wa kikundi
(iv)
Kikundi: Taasisi hii inayoanzishwa kwa mujibu wa katiba ambayo inatambulika kuwa ni
UMOJA.
(v)
Matatizo:Ina maana ya misiba kwa mujibu wa katiba hii.
(vi)
Nidhamu: Kitendo chochote kile kinacho kinzana na Katiba hii pamoja na kanuni zake.
SURA YA PILI
2.1
AINA YA KIKUNDI
PAMOJA
TUNAWEZA ni Kikundi cha Kijamii cha Kimaendeleo ya Kiuchumi (Community
Based Organisation)
2.2
MADHUMUNI NA MALENGO YA KIKUNDI.
Kikundi hiki kipo kwa kutimiza au kutekeleza
yafuatayo..
(i)
Kushirikiana kufanya
miradi mbalimbali ya Kiuchumi na Kijamii kwa maendeleo ya kikundi na ustawi wa wanachama
(ii)
Kuanzisha mfuko wa kikundi
wa kuweka na kukopa.
(iii)
Kushirikiana na kusaidiana nyakati za shida
na raha.
(iv)
Wanakikundi kuwezeshana katika
kuimarisha hali zao za Kipato ili kuweza kuwa na maisha yaliyo bora zaidi.
(v)
Kuwezesha kifedha shughuli binafsi za
Wanakikundi mmoja mmoja kwa kuzingatia Masharti na Kanuni zitakazokuwa
zimeafikiwa na Wanakikundi wote.
2.3. MATARAJIO YA KIKUNDI
Ili kuweza kufikia matarajio ya
Kikundi kitafanya yafuatayo:-
·
Kuweka
utaratibu mahsusi MICHANGO YA FEDHA kwa wanakikundi ikiwa ndio msingi wa chanzo
cha mapato.
·
Kubuni
Miradi mbalimbali itakayosimamiwa na kuendeshwa Wanakikundi wenyewe au hata kwa
msaada wa kiufundi kutoka nje ya kikundi.
·
Kuweza
kuandaa maandiko ya kuwezesha kuomba MISAADA kutoka kwa Washirika mbalimbali wa
Maendeleo wa ndani na nje ya Tanzania.
·
Kuimarisha
Ushirikiano na Wanakikundi wenye changamoto mbalimbali kama vile; Maradhi,
Misiba,Harusi na Sherehe, Majanga ya Kiasili na matukio mengine yanayolingana
na hayo.
taratibu hizo zitakuwa ni sehemu ya Katiba hii.
SURA YA TATU
3.0 UANACHAMA.
Kutakuwa na aina
mbili zifuatazo za uanachama ambazo ni;
3.1.1.
Mwanachama wa
Kawaida
Ni mtu
yeyote yule ambaye ametimiza taratibu
zote za kujiunga na Kikundi au Umoja huu kwa mujibu wa Katiba na Kanuni zake
ikiwa ni pamoja na kulipa Ada na Michango stahiki.
3.1.2.
Mwanachama wa
Kutunukiwa
Mwanachama wa
Kutunukiwa ni Mtu yeyote atakaetunukiwa uanachama kupitia maamuzi au azimio la
Mkutano Mkuu katika kuthamini Mchango uliotolewa na Mtu huyo ama atakaoendelea
kuutoa kwa kuleta maendeleo na ufanisi wa Malengo ya Kikundi au Umoja huu.
3.2.1
Sifa za kuwa Mwanachama
(i)
Awe na Umri usiopungua
miaka 18.
(ii)
Awe mwenye nia na awe
tayari kuwa mwanachama
(iii)
Awe tayari kushiriki
kikamilifu kwenye shughuli za kikundi
(iv)
Awe na akili timamu.
(v)
Awe tayari kutii na kufuata masharti ambayo yameainishwa kwenye Katiba
na Kanuni za kikundi
(vi)
Awe tayari kulipa
kiingilio pamoja na ada ya uanachama ya kila mwezi
3.3.1 Haki za Mwanachama
(i)
Kutoa maoni yake kwa uhuru
(ii)
Kuchagua
au kuchaguliwa katika nafasi yoyote ile ya Uongozi katika Kikundi au Umoja huu.
(iii)
Kuwasiliana
na Uongozi/Viongozi ikiwa ni pamoja na kupokea na kutoa taarifa zinazohusu Kikundi
au Umoja huu.
(iv)
Kuhudhuria
na/au kuwakilisha katika jambo lolote lile linalohusu Kikundi au Umoja huu kwa
kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba hii.
(v) Kupewa
nafasi ya kujieleza na kujitetea pindi anapokabiliwa na tuhuma zozote zile
dhidi yake katika umoja huu.
(vi)
Kutumia Mali za Kikundi kwa kufuata
utaratibu na Kanuni za Umoja huu.
(vii) Ana
haki ya kutoa hoja yake na kusikilizwa wakati wa kushiriki majadiliano kwenye
vikao.
(viii)
Kufahamu
mapato na matumizi ya Kikundi kwa kutumia na kuzingatia Kanuni.
(ix)
Kusaidiwa
linapomtokea tatizo.
(x)
Kusaidiwa kimawazo au kiuchumi kulingana na hali itakavyo ruhusu.
3.3.2
Wajibu wa Mwanachama.
(i)
Kuilinda na kuitetea
katiba hii wakati wote.
(ii)
Kutekeleza majukumu atakayopewa
na viongozi au wanachama wenzake.
(iii)
Kushiriki katika shughuli
zote za kikundi kwa mujibu wa katiba hii ikiwa ni pamoja na vikao halali vya
Umoja huu.
(iv)
Kulipa ada pamoja na
michango mbalimbali itakayo pitishwa na Kikundi au Umoja huu.
(v)
Kueneza sifa nzuri za Umoja huu.
(vi)
Kutii na kufuata maagizo na maazimio ya
Mkutano/Mikutano halali ya Umoja huu, hata ikiwa hatakuwepo kwenye Mkutano huo,
au hakushiriki katika kupitisha azimio hilo.
(vii)
Kuwa na nidhamu wakati wa Mikutano ama
shuhuli nyingine zozote za Kikundi.
(viii)
Kutunza siri zote za Umoja huu
3.4.1
Kujiunga na Kikundi.
(a) Kujaza
Fomu ya maombi itakayotolewa kwa ada itakayokuwa imepangwa.Maombi haya ni
lazima yapitiwe na kukubaliwa na Uongozi, kisha kupitishwa na MkutanoMkuu au
Mkutano Mkuu Maalum.
(b) Baada ya kukubaliwa Mwombaji atatakiwa
kulipa Ada ya kiingilio cha kiasi kitakachokuwa kimepangwa na Mkutano Mkuu au
Mkutano Mkuu Maalum kwa wakati huo.
(c) Pamoja
na Ada ya kiingilio Mwanachama mpya atalazimika kulipa Mchango wa Miezi Miwili
au zaidi Ili aweze kuwa Mwanachama kamili wa Kikundi.
3.4.2 MICHANGO
(a) ADA YA UANACHAMA
Kila Mwanachama
atalazimika kulipa ada ya Uanachama kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 3.4.1.(b)
na (c) ya Katiba hii.
ILI
MRADI IELEWEKE KWAMBA:-
Mwanachama ambaye alikuwa na taarifa juu ya uanzishwaji wa kikundi na hakujiunga wakati
huo, endapo atataka kujiunga baadae, atatakiwa kulipa kiingilio na michango
yote tangu kikundi kilipoanza mpaka kilipofikia, ndipo ataweza kukubaliwa kuwa
mwanachama.
(b)
MICHANGO MINGINEYO.
Kila Mwanachama atawajibika
kuwasilisha mchango mwingine wowote ule utakaoamuliwa kuchangishwa kwa azma
ya kukidhi miongoni mwa matarajio ya Umoja huu kama yalivyoainishwa katika
ibara 2.3 ya Katiba hii na kima kitakachokuwa kimeamuliwa.
(c) MICHANGO
YA HIARI
Kutakuwa na michango ya hiari ambayo mtu
hatolazimishwa bali anaweza kujitolea mali au fedha kwa mapenzi yake
mwenyewe kwa lengo la kukijenga na
kukiendeleza Kikundi.
3.4.3 Kukoma Uanachama.
Mwanachama anaweza kukoma kuwa mwanachama katika
mazingira yafuatayo:-
(i)
Kujitoa kwa hiari yake kwa
kutoa taarifa ya maandishi kwa mwenyekiti wiki moja kabla na kama ana mali za
Kikundi atalazimika kurudisha ndipo atakubaliwa kutoka, lakini hatorudishiwa
michango au mali yoyote aliyoitoa kwa ajili ya Kikundi.
(ii)
Kushindwa kulipia ada ya
kila mwezi kwa miezi mitatu mfululizo bila sababu yoyote ya msingi.
(iii)
Kutohudhuria bila taarifa
vikao vitatu mfululizo vilivyowekwa kwa mujibu wa katiba hii bila sababu ya
msingi.
(iv)
Kupuuza taarifa zinazotaka
ushiriki wake katika shughuli za wanachama.
(v)
Kupoteza sifa kutokana na
mambo ya kinidhamu
(vi)
Ikiwa mwanachama atafariki.
(vii)
Kushidwa kufuata Katiba na Kanuni za Kikundi.
ILI
MRADI IELEWEKE KUWA
Mtu aliyeacha au kufukuzwa
Uanachama(uanakikundi) anaweza kuomba kujiunga tena kwa mujibu wa masharti ya
uanakikundi baadae na atatakiwa kuwa na wadhamini wasiopungua WATATU ndani ya
Kikundi ambao ni hai.
NA
Kama mwanachama atakoma
kutokana na vigezo tajwa hapo juu, atakuwa amepoteza haki zake zote za msingi kama mwanachama.
SURA YA NNE.
4.0 UONGOZI.
4.1
Kikundi hiki kitakuwa na
viongozi wafuatao:-
(i)
Mwenyekiti
(ii)
Makamu Mwenyekiti
(iii) Katibu
(iv)
Katibu Msaidizi
(v)
Mweka Hazina
4.2 Kikundi
kitakuwa na kamati zifuatazo.
4.2.1 Kamati ya Utendaji.
Itakayoundwa na wajumbe wafuatao:-
1.
Mwenyekiti
2.
Makamu Mwenyekiti
3.
Katibu
4.
Katibu Msaidizi
5.
Mweka Hazina
6.
Wajumbe wawili watakaochaguliwa
na Mkutano Mkuu.
4.2.2 Kazi
za Kamati ya Utendaji.
(i)
Kusimamia utekelezaji wa
maamuzi ya vikao halali vya Kikundi au Umoja huu.
(ii)
Kukutana wakati wa dharura
na kujadili suala lilipo mbele yao na kulitolea uamuzi kwa niaba ya wanachama
wote.
(iii)
Kuandaa agenda za mkutano
mkuu.
(iv)
Kuandaa taarifa mbalimbali
kwenye mkutano mkuu.
(v)
Kasimamia shughuli zote za
kimaendeleo na ukuaji wa taasisi
(vi)
Kujadili na kuyafanyia
kazi mambo mbali mbali yanayohusu wanachama au Kikundi kwa ujumla wake.
4.2.3 Kamati
ya Fedha na Mipango
Kamati hii itaundwa na wajumbe watano watakao teuliwa na mkutano mkuu
wa kikundi. Wajumbe wa kamati hii watachagua kutoka mingoni mwao na kumpata Mwenyekiti
na Katibu siku ya kikao cha kwanza cha kamati hii.
4.3.2 Kazi
za Kamati ya Fedha na Mipango
(i) Itakayokuwa na kazi ya kubuni, kushauri
na kuelekeza juu ya miradi yote ya kimaendeleo ya kikundi hiki.
(ii)
Itakuwa na kazi ya kusimamia utekelezaji wa miradi na mambo yote ya
fedha ya kikundi
(iii) Kudhibiti na kusimamia mapato na matumizi
ya fedha na mali za kikundi kwa kufuata Kanuni zilizowekwa.
4.2.4 Kamati ya Sheria na Nidhamu
Kamati hii itakuwa na jukumu la kusimamia nidhamu na kushughulikia
migogoro ya wanachama. Kamati hii itaundwa na wajumbe watatu watakaoteuliwa na
wana kikundi. Mwenyekiti wake kama itawezekana awe ni mtu mwenye elimu ama ufahamu wa sheria. Kama hatakuwepo mtu wa
kukidhi kigezo hicho, mtu mwingine yeyote atakayeteuliwa na wanakamati wenyewe
ndio atakuwa Mwenyekiti.s
SURA YA TANO.
5.0
KAZI ZA VIONGOZI
5.1
Kazi za Mwenyekiti.
(i)
Atakuwa msemaji mkuu wa
kikundi.
(ii)
Ataitisha mikutano yote ya
kikundi.
(iii)
Ataitisha mkutano wa
dharura pale itakapokuwa inahitajika.
(iv)
Ataongoza mikutano yote ya
wanachama wote.
(v)
Atakuwa ndio Kiongozi Mkuu
wa Kikundi au Umoja huu.
5.2
Kazi za Makamu Mwenyekiti.
(i)
Atafanya kazi zote za
Mwenyekiti pale ambapo Mwenyekiti hatakuwepo.
(ii)
Atafanyakazi zote
atakazoelekezwa na Mwenyekiti.
(iii)
Atakuwa ndio msaidizi mkuu
wa Mwenyekiti.
5.3
Kazi za Katibu.
(i)
Atakuwa Mtendaji Mkuu wa
kikundi.
(ii)
Kuandaa ajenda za vikao
vyote.
(iii)
Ataandika miniti za vikao
vyote vya kikundi.
(iv)
Atakuwa anatoa taarifa ya
maendeleo ya kikundi mara moja kwa mwezi
(v)
Kwa kushirikiana na Mwenyekiti
atakuwa anaandaa yatokanayo na vikao vilivyopita
(vi)
Atakuwa mtunza kumbukumbu
na nyaraka mbalimbali za kikundi.
(vii)
Atakuwa katibu wa kamati
ya utendaji.
(viii)
Atakuwa mjumbe wa kamati
ya Fedha na Mipango.
(ix)
Atawajulisha wanachama
taarifa zote za vikao.
(x)
Atafanya kazi zote kadri
atakavyoelekezwa na Mwenyekiti.
5.4
Kazi za Katibu Msaidizi .
i.
Atamsaidia Katibu
kuendesha shughuli za kila siku za kikundi.
ii.
Atakaimu nafasi ya Katibu pale ambapo Katibu atakuwa hayupo.
(i)
Atakuwa mtunza fedha za
kikundi.
(ii)
Atakusanya / atapokea
fedha zote za kikundi na kutoa
stakabadhi.
(iii)
Atakuwa mtunza nyaraka
zote zinazohusiana na masuala ya fedha.
(iv)
Atatoa taarifa ya mapato
na matumizi ya kikundi kila miezi mitatu.
(v)
Atafanya malipo yote halali ya kikundi.
(vi)
Atajibu hoja zote zinazo husiana
na masuala ya fedha.
(vii)
Atakuwa mjumbe wa kamati
ya utendaji pamoja na kamati ya Fedha na Mipango.
SURA YA SITA.
6.0
VIKAO
Kikundi hiki kitaongozwa
kwa kufanya vikao mbali mbali kama vifuatavyo.
6.1
Mkutano Mkuu
Kutakuwa na mkutano mkuu utakaofanyika mara moja kwa mwaka. Ili mkutano huu ufanyike idadi ya wajumbe watakohudhuria kikao
hicho ni lazima iwe siyo chini ya asililimia
HAMSINI (50%) ya wajumbe wote walio hai
6.2
Kazi za Mkutano Mkuu.
(i)
Kuchagua viongozi wa
kikundi.
(ii)
Kupokea taarifa za mapato
na matumizi kwa mwaka mzima.
(iii)
Kupokea taarifa ya kazi
zote za mwaka.
(iv) Kufanya mabadiliko au marekebisho kwenye vifungu
mbalimbali vya katiba.
(v) Kuidhinisha mipango ya kimaendeleo ya kikundi
(vi) Kufanya Uchaguzi wa viongozi ikiwa muda umewadia.
6.3
Mkutano wa Kawaida wa
Wanachama Wote.
Mkutano huu utafanyika mara moja kwa mwezi, siku
na tarehe zitajulishwa na katibu wiki
moja kabla.
Ili
mkutano huu ufanyike ni lazima idadi ya wajumbe ifikie asililimia 50% ya
wajumbe wote walio hai. Endapo kikao kitasitishwa mara mbili kwa kukosa akidi, kikao
cha tatu kitaendelea hata kama akidi
itakuwa haijafikiwa na maamuzi ya kikao yatakuwa maamuzi halali ya
kikundi.
6.4
Kazi za Mkutano wa Kawaida
wa Wanachama Wote.
(i)
Kupokea taarifa ya utendaji na uendeshaji
kikundi kwa mwezi husika.
(ii)
Kukusanya michango ya kila
mwezi toka kwa wanachama.
(iii)
Kupata taarifa za
utekelezaji wa maagizo na malengo yoyote ya kikundi.
(iv)
Kupokea taarifa ya fedha
ya mwezi husika.
(v)
Kupitisha maamuzi ya
kamati mbalimbali za kikundi.
(vi)
Kujadili na kulitolea
uamuzi suala lolote litakalokuwa limejitokeza.
(vii) Kupanga tarehe na sura ya kufanyia mkutano wa mwezi
unaofuata.
6.5
Kikao cha Kamati ya Utendaji.
Kutakuwa na vikao vya mara kwa mara vya kamati ya
utendaji kadri itakavyohitajika.
Kazi za vikao hivi ni kama ilivyoonyeshwa kwenye kifungu cha
4.2.2 cha katiba. Ili
vikao hivi vifanyike ni lazima idadi ya wajumbe wa kamati wafikie asililimia
50% ya wanakamati ya utendajiti walio hai.
6.6 Kikao cha kamati ya Fedha na Mipango.
Kamati hii itakua na vikao
kadri itakavyohitajika kufanya hivyo, ili vikao hivi
vifanyike ni lazima idadi
ya wajumbe wa kamati wafikie asililimia 50% ya wanakamati wote
walio hai
6.7 Kazi za vikao vya kamati ya Fedha na Mipango.
(i)
Kuandaa Mpango wa Mkakati
wa Kikundi
(ii) Kubuni miradi kwa ajili ya kuongeza mapato ndani ya Kikundi.
(iii) Kutoa ushauri elekezi na kitaalamu juu ya miradi
mbalimbali ya Kikundi
(iv)
Kusimamia miradi
mbalimbali ya kikundi na kuandaa taarifa za maendeleo.
(v)
Kujadili maombi yote ya
mikopo na kutoa mapendekezo yake kwa Mwenyekiti.
(vi) Kuandaa taarifa za ukusanyaji madeni yote toka kwa wanachama.
SURA YA SABA
7.0
TARATIBU ZA UCHAGUZI
Kutakuwa na chaguzi mbali
mbali za viongozi wa kikundi, ambazo zitafanyika kila baada ya
miaka miwili(2) katika Mkutano
Mkuu wa Kikundi wa mwaka. Kama ifuatavyo:-
7.1
Mwenyekiti na Makamu
Mwenyeki wa kikundi.
(i)
Watachaguliwa kwa kura ya
siri.
(ii) Kutoka miongoni wa wajumbe wa kikundi yatapendekezwa
majina matatu na kupigiwa kura kwa pamoja,
ambapo Mwenyekiti na makamu wake
watapatikana kutokana na wingi wa
kura utakao patikana. Ambapo atakaye pata kura
nyingi zaidi ya mwenzake ndiye atakuwa
amechaguliwa kama Mwenyekiti wa kikundi na
atakayefutia kwa wingi wa kura atakuwa
Makamu Mwenyiki.
7.2
Katibu wa Kikundi
(i)
Atachaguliwa kwa kura ya siri.
(ii)
Kutoka miongoni mwa
wajumbe wa kikundi yatapendekezwa majina matatu na kupigiwa kura kwa pamoja.
Katibu atapatikana kutokana na wingi wa kura atakazopata, ambapo atakaye pata
kura nyingi zaidi ya mwenzake ndiye atakuwa amechaguliwa kama Katibu wa
kikundi. Atakayefutia kwa wingi wa kura atakuwa Katibu Msaidizi
7.3
Mweka Hazina wa kikundi
(i) Atachaguliwa kwa kura ya siri.
(ii) Kutoka miongoni mwa wajumbe wa kikundi yatapendekezwa
majina matatu na kupigiwa kura kwa pamoja. Mweka hazina atapatikana kutokana na
wingi wa kura atakazopata. Atakaye pata
kura nyingi zaidi ya wote ndiye atakuwaamechaguliwa mweka hazina wa kikundi.
SURA YA NANE
8.0
ADA
8.1
Kutakuwa na michango na
ada mbali mbali ambazo zitaainishwa
kwenye kanuni za kikundi . Michango na ada hizo ni kama ifuatavyo:
i.
Kiingilio kwa wanachama
ii.
Ada ya kila mwezi kwa kila
mwanachama,
iii.
Ada nyingine kama itakavyoamuliwa
na wanachama kufuatana na katiba na kanuni za kikundi.
SURA YA TISA
9.0
UTUNZAJI FEDHA BENKI
Kikundi kitatunza fedha zake kwenye benki
itakayopitishwa na Mkutano Mkuu.
Fedha zitatolewa kwenye akaunti kwa mujibu wa taratibu
zilizo wekwa kwenye kanuni za fedha za kikundi.
SURA YA KUMI
10.0
UTATUZI WA MIGOGORO
Ufuatao ni utaratibu wa kikundi kutatua migogoro
itakayo jitokeza ndani ya kikundi:
Migogoro yote ya kikundi itatatuliwa Kamati ya Sheria na Nidhamu. Kama Mgogoro huo utashindikana kutatuliwa na Kamati ya Sheria na
Nidhamu mgorogoro huu utapelekwa
(i) Kamati ya utendaji
(ii) Kupelekea mgogoro
huo kwa msajili wa vyama, kwa kufuata utaratibu uliowekwa.
(iii) Kupeleka mgogoro mahakamani kwa kufuata taratibu za kisheria.
Gharama za utatuzi wa mgogoro au shauri lililofunguliwa
zitalipwa na aliyefungua/ waliofungua mgogoro au shauri hilo. Kikundi hakitahusika na gharama zozote za
usuluhishi wa mgogoro husika.
(iv) Na endapo
mwanachama/ wanachama watakataa kufuata
makubaliano ya utatuzi wa
shauri, basi watakuwa wamejifukuzisha
uwanachama wao wenyewe /mwenyewe/na kupoteza haki zao za msingi.
SURA YA KUMI NA
MOJA
11.0
KUBADILI KATIBA.
Mabadiliko yeyote ya katiba yatafanyika baada ya
kupitishwa na mkutano mkuu wa kikundi wa mwaka ambao unafanyika mara moja kwa
mwaka. Mabadiliko yatapitishwa kwa kupigiwa kura ya wazi na zaidi ya asilimia
50% ya wanachama wote waliohai. Katiba itakuwa inafanyiwa marekebisho na
kupitishwa upya kila baada ya miaka mitatu, au pale ambapo itaonekana
kuna haja ya kufanya hivyo
SURA YA KUMI NA MBILI
12.0
KUVUNJIKA KWA KIKUNDI.
(i)
Kikundi kitakuwa
kimevunjika endapo asilimia 80% ya wanachama hai watapiga kura ya
ndio ya kuvunja kikundi katika mkutano mkuu wa
kikundi.
(ii) Endapo kikundi kitafutwa na Msajili wa Vyama.
(iii) Endapo kikundi kitavunjika kila mwanachama atakuwa na
haki sawa ya kurudishiwa
michango
yake kulingana na hali ya fedha itakavyokua.
Mali yote iliyopatikana itagawanywa sawa kwa kila mwanachama.
SURA YA KUMI NA TATU
13.0
HITIMISHO:
Katiba hii imesomwa, kujadiliwa na kupitisha na wanachama
wote. Na kuweka sahihi kwa niaba yao na:
Mwenyekiti wa kikundi Katibu wa Kikundi
Jina MULHAT .A. SAIDI Jina MAULID
SONGAMBELE
Sahihi................................... Sahihi
…………………….……
Tarehe ………………………… Tarehe
………………………
MAJINA YA WANACHAMA
WAANZILISHI SAHIHI YA MWANACHAMA
1.
MBAROUK .H. SALIM
---------------------------
2.
JUMA .F. MASOUD ---------------------------
3.
KHAMIS .S.YUSUPH ----------------------------
4.
RASHID.S.KIHANZA ---------------------------
5.
ALHAJ .M. DOLE
----------------------------
6.
ISLAM ISLAM
----------------------------
7.
MAULID SONGAMBELE ---------------------------
8.
SHABANI AKILI -----------------------------
09.
MULHAT AHMED ----------------------------
10.
ROSE RAMADHAN -----------------------------
11.
SAIDA AHMED --------------------------------
12.
KURTHUMU SHABANI -------------------------------
13.
MARIAM RAHIM -------------------------------
14.
ZANNA ABDILLAH --------------------------------
15.
MWARAHA TEWA --------------------------------
16.
NASRA SHABANI ----------------------------------
17.
MWAJUMA SHISHA ---------------------------------
18.
ASHA MDAHOMA ----------------------------------